Mshambuliaji alilenga watumiaji mitandao ya kijamii
16 Machi 2019Alionesha moja kwa moja mauaji hayo, akipiga kelele kauli mbiu maarufu na kuchapisha rasimu ndefu ikiwa na utani ndani yake iliyolenga wale waliojificha chini kwa chini katika utamaduni wa mtandao wa internet.
Hii yote inamfanya Brenton Harrison Tarrant , mtu aliyeshitakiwa kwa mauaji kuhusiana na shambulio hilo la Ijumaa katika misikiti mjini Christchurch, mtu wa hivi karibuni kabisa kudaiwa kufanya mauaji makubwa pamoja na wito kwa jamii ya mitandao ambayo inazalisha itikadi kali.
Kabla ya kuuwawa watu sita mjini Isla Vista, Califonia, mwaka 2014, Elliott Rodger aliweka mtandaonmi vidio na kusambaza waraka mrefu ukiwa na malalamiko kadhaa. Baadaye aligundulika kuwa na mahusiano na kundi la mtandaoni la misogynisti linalofahamika kama "Incels" ama "Involuntary celibates," ambao baadhi ya nyakati hutoa wito wa matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake. Mwaka jana Robert Bowers, mtu aliyeshitakiwa kwa kuwauwa watu 11 katika sinagogi la mjini Pittsburgh , aliweka mtandaoni vitisho dhidi ya Gab, tovuti ya mtandao wa kijamii unaopendelewa na wazungu wanaoamini kuwa wao ni jamii bora, White suprimacists.
Uandikishaji pamoja na kusambaa kwa mawazo ya itikadi kali si kitu kipya, kwa mtu ama katika mitandao. Watu ambao wanataka kujadili mawazo kama hayo yanauwezo wa kujuana, amesema Daniel Byman, mtaalamu mwandamizi katika taasisi ya Brookings. Lakini wakati makundi madogo huenda yamekutana mar moja katika maisha halisi, sasa watu wanaweza kwenda katika mtandao na kukutana na makundi makubwa kujiimarisha na kuendeleza mawazo yao karibu wakati huo huo.
Matendo ya mtandaoni
Watu hufanya mambo katika mtandao ambayo wanaweza kusita kufanya katika maisha halisi, Byman amesema. Hii inaweza kuwa kuanzia matendo ambayo hayana madhara, kama kutuma barua pepe kwa mtu ambae huwezi kukutana nae katika hafla, na kubadilishana nae mambo, kujenga na kuhimiza mawazo ya itikadi kali pamoja na matumizi ya nguvu.
"Inakuwezesha kuwa jasiri," Byman amesema.
Wapelelezi mtandaoni haraka waliweza kuhusisha na video hiyo iliyoonekana moja kwa moja na maandishi yaliyotolewa na mtumiaji huyo katika 8chan, kona ya kificho ya tovuti ambako wale ambao hawaridhishwi na mitandao ya kijamii inayofahamika mara nyingi huweka maandishi yao ya mawazo ya imani kali , kibaguzi na matumizi ya nguvu.
Waraka wa Tarrant ulisambaa haraka katika 8chan jana Ijumaa. Waraka huo wenye kurasa 74 unasambaza mawazo ya wazungu wanaoamini kuwa wao ni jamii bora hata kama unajikanganya wenyewe. Baadhi waliona hali ya kushabihiana katika waraka wa kurasa 1,500 ulioandikwa na Anders Behring Breivik, Mnorway mwenye hisia za siasa kali za mrengo wa kulia ambaye aliwauwa watu 77 katika mwaka 2011.
Waraka
Waraka wa Tarrant unaonekana kulenga kutoa kwa jamii ya mtandaoni aliyoshiriki , kwa sehemu kwa kueleza mada zinazofahamika sana katika mtandao wa internet na mitazamo wa kejeli.
Rais Donald Trump wa Marekani ameonesha hali ya kupuuzia kuwapo na kitisho kinachotokana na uzalendo wa kibaguzi wa wazungu baada ya mtu huyo aliyekuwa na silaha na kufanya mauaji katika misikiti nchini New Zealand kumuita rais huyo kuwa "ni ishara ya utambuzi mpya wa wazungu".
Trump ambaye hatua zake za kushughulikia vuguvugu hilo la wazungu zilisababisha kuangaliwa kwa undani, ameeleza kusikitishwa kwake na wahanga waliouwawa , katika kile alichosema "maeneo ya ibada yaliyogeuzwa maeneo ya mauaji ya uovu. lakini amekataa kujiunga na maelezo ya ongezeko la wasi wasi juu ya uzalendo wa kizungu, wakati alipoulizwa iwapo anafikiri ni kitisho kinachoongezeka duniani, alijibu , "sifikiri hivyo kwa kweli.
Wakaazi wa New Zealnad walioshitushwa na tukio la mauaji walifika katika maeneo wanakoishi jamii ya Waislamu katika nchi hiyo leo Jumamosi, katika dhamira nzito kuonesha ukarimu wakati mtu aliyefyatua risasi mwenye imani ya kuwa jamii ya wazungu ndio jamii bora akisimama kimya mbele ya jaji , akishutumiwa kwa mauaji katika misikiti ambapo watu 49 waliuwawa.