1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msaada wa chakula waongezeka Darfur lakini hautoshi - WFP

21 Juni 2024

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema jimbo la Darfur limeshuhudia ongezeko la msaada wa chakula unaohitajika, lakini likaonya kwamba kiwango hicho bado hakitoshi kuzuia baa la njaa.

https://p.dw.com/p/4hLqN
Darfur Sudan
Mkimbizi wa Darfur akiwa na mwanawe.Picha: Albert Gonzalez Faran/Unamid/Han/dpa/picture alliance

Katika taarifa yake, WFP imesema kuwa tangu mwanzoni mwa mwaka 2024, misafara mitano iliyobeba karibu tani 5,000 za msaada wa chakula imevuka kutoka nchi jirani ya Chad hadi eneo la Darfur linalokumbwa na mzozo wa kijeshi. 

Mkuu wa mawasiliano katika ofisi ya WFP nchini Sudan, Leni Kinzli, ameliambia shirika la habari la AP kwamba usambazaji wa chakula unaendelea katikati mwa Darfur na magharibi mwa jimbo hilo "na kwamba hiyo ni hatua ya dharura ili kuepusha baa la njaa kote nchini humo.