1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mripuko wauwa watu wanane Pakistan

25 Aprili 2023

Watu wanane wamekufa baada ya kutokea milipuko kwenye ofisi ya kupambana na ugaidi mjini Peshawar, kaskazini magharibi mwa Pakistan.

https://p.dw.com/p/4QW1l
Pakistan Blast
Picha: Sherin Zara/AP/picture alliance

Watu wengine zaidi ya 50 walijeruhiwa. Hata hivyo mkuu wa polisi wa jimbo Akhtar Hayat amesema, kilichosababisha milipuko hiyo bado hakijajulikana kwenye sehemu hiyo ambayo hapo awali ilikuwa inadhibitiwa na magaidi. Magaidi hao ndiyo waliompiga risasi na kumjeruhi mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Malala Yousafzai mnamo mwaka 2012. Idadi kubwa ya waliouawa katika milipuko hiyo miwili walikuwa polisi wa kikosi cha kupambana na ugaidi. Mama mmoja na mwanawe waliokuwa wapita njia pia waliuawa. Uchunguzi unafanyika ili kubainisha iwapo milipuko hiyo ilisababishwa na zana zilizokuwa zimewekwa kwenye stoo au lilikuwa shambulio la kigaidi.Mkuu wa idara ya kupambana na ugaidi ameeleza kuwa silaha zimewekwa katika stoo hiyo.