1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpinzani wa mradi wa TotalEnergies aachiliwa huru

10 Juni 2024

Mwanaharakati wa mazingira nchini Uganda ambaye anapinga mradi mkubwa wa mafuta unaoongozwa na kampuni ya Ufaransa ya TotalEnergies Stephen Kwikiriza ameachiliwa huru baada ya kuwa kizuizini kwa siku tano.

https://p.dw.com/p/4gsC4
TotalEnergies
Picha ikionyesha maeneo yanayofanyiwa shughuli za kampuni ya mafuta ya TotalEnergiesPicha: Waltraud Grubitzsch/dpa/picture alliance

Mkurugenzi wa Taasisi ya Usimamizi wa Mazingira, Samuel Okulony, ambaye ni muajiri wa Kwikiriza amesema walimpata mwanaharakati huyo kando ya barabara huko Kyenjojo, takribani mwendo wa saa tano kwa gari magharibi mwa mji mkuu Kampala.

Okulony ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wanaharakati huyo amemwaambia kwamba alipigwa na maafisa wa jeshi na sasa anatibiwa katika hospitali ya Kampala.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani yaliibua wasiwasi kuhusu hatima ya Kwikiriza baada ya kutoweka siku ya Jumanne.

Shirikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu (FIDH), limesema wanaharakati 11 wa mazingira walitekwa nyara, kukamatwa kiholela, kuzuiliwa au kufanyiwa aina mbalimbali za unyanyasaji na mamlaka ya Uganda kati ya Mei 27 na Juni 5, 2024.