Mpango wa UK kuwapeleka wahamiaji Rwanda waenda mahakamani
5 Oktoba 2023Matangazo
Mawakili wa serikali watahoji kwamba hukumu hiyo ilikuwa ya makosa. Kwa upande wao wanaowawakilisha wahamiaji kutoka Syria, Iraq, Iran na Sudan wanawataka majaji wabakie na msimamo uleule kwamba mpango huo wa kuwahamisha wahamiaji wa serikali ya Uingereza ulikuwa wa makosa.
Waziri mkuu Rishi Sunak na mawaziri wake wanahoji kwamba mpango huo wa kuwahamishia wakimbizi nchini Rwanda uliozinduliwa mwaka uliopita na waziri mkuu wa hapo awali Boris Johnson utaivunja biashara ya wahalifu wanaosafirisha binadamu.