1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa kugawa maji waanza Cape Town

29 Januari 2018

Mji wa watalii wa Cape Town nchini Afrika Kusini umeanza operesheni ya kujiandaa na janga, Aprili 12, siku ambayo inakadiriwa mji huo utakuwa bila ya maji, kutokana na ukame.

https://p.dw.com/p/2rgzn
Wasserknappheit in Südafrika
Picha: Julia Jaki

Maafisa 86 wa jiji hilo watatoa muongozo juu ya mpango huo ambapo watagusia juu ya vituo 200 vya usambazaji maji ambapo wakaazi wataweza kupata tu lita 25 za maji kwa kila mtu, kila siku, kukiwa na ukaguzi wa polisi na wanajeshi. 

Msimu wa mvua unatarajiwa kuanza mwezi Mei hadi Juni, huku hadi wakati huo, Cape Town ikisalia kuwa na uhaba mkubwa wa maji.