Moto wauwa 27 Istanbul
2 Aprili 2024Matangazo
Moto huo ulianzia chini katika jengo hilo la makaazi ya watu lenye ghorofa 16 kwenye sehemu hiyo hutumiwa kama klabu ya usiku.
Gavana wa jiji hilo, Davut Gul, aliwaambia waandishi wa habari katika eneo la tukio kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na uchunguzi unaendelea, lakini akasema kuwa inaaminika miongoni mwa waliokufa ni watu waliokuwa wakihusika na kazi za ukarabati.
Soma zaidi: Erdogan aahidi kurekebisha makosa baada ya kushindwa uchaguzi Uturuki
Waziri wa Sheria wa Uturuki, Yilmaz Tunc, amesema wanawashikilia watu watano kwa mahojiano, wakiwemo mameneja wa klabu hiyo na mtu mmoja aliyekuwa akisimamia ukarabati huo.