1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moto wa nyika mjini Los Angeles Marekani waharibu majengo

8 Januari 2025

Majengo mengi mjini Los Angeles nchini Marekani yameharibiwa na moto mkubwa wa nyika unaozidi kushika kasi na kusababisha msongamano mkubwa wa magari siku ya Jumanne.

https://p.dw.com/p/4ow8P
Marekani Los Angeles 2025 | Moto wa nyika
Moto wa nyika Los AngelesPicha: Eugene Garcia/AP Photo/picture alliance

Majengo mengi mjini Los Angeles nchini Marekani yameharibiwa na moto mkubwa wa nyika unaozidi kushika kasi na kusababisha msongamano mkubwa wa magari siku ya Jumanne.

Zaidi ya watu elfu 30,000 wamehamishwa wakati moto mwingine ukiongezeka maradufu umbali wa maili 30. Mkuu wa kikosi cha zimamoto katika eneo hilo Antony Marrone amesema kwamba. 

"Bado tuko hatarini. Idara ya Hali ya Hewa ya Kitaifa imetabiri kuwa upepo utaongezeka na kuwa mbaya zaidi. Tutakuwa na upepo mkali kati ya saa 10 jioni na 5 asubuhi kesho. Kwa hivyo ni wajibu wa kila mtu kuwa na mpango wa kukabiliana na moto wa nyika katika nyumba zao ikiwa wanaishi katika eneo lililozingirwa na moto.

Soma: Maelfu watumwa kuukabili moto wa nyika California

Maafisa wanasema hekari zaidi ya 2,900 za ardhi baina ya miji ya pwani ya Santa Monica na Malibu zimeteketezwa kwa moto.