1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moroko yaiangusha Liberia 3-0 kuelekea AFCON 2024

Josephat Charo
18 Oktoba 2023

Timu ya taifa ya Moroko imeifunga timu ya taifa ya Liberia 3-0 kwenye mechi ya kuwania ushiriki wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2024.

https://p.dw.com/p/4Xfv8
Fußball Finale der afrikanischen Champions League 2023
Mechi kati ya timu ya Wydad ya Moroko na Al Ahly ya Misri.Picha: Mosa'ab Elshamy/AP/picture alliance

Amine Harit, Ayoub El Kaabi na Amine Adli walifunga mabao wakati Moroko ilipoishinda Liberia 3-0 katika mji wa bandari wa kusini wa Agadir siku ya Jumanne (Oktoba 17)  katika mechi ya mwisho ya kufuzu kwa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Soma zaidi: Wenyeji wa AFCON Ivory Coast wapangwa kundi moja na Nigeria

 Awali mechi hiyo ya Kundi K ilikuwa imepangwa kuchezwa Septemba lakini ikaahirishwa baada ya tetemeko la ardhi lililotokea kiasi kilometa 250 kutoka Agadir kuwaua watu 3,000.

Moroko na Afrika Kusini zilikuwa tayari zimeshafuzu tangu mwezi Juni kwa michuano hiyo itakayoanza Januari 13 hadi Februari 11 nchini Ivory Coast, katika ligi ndogo iliyozishirikisha timu tatu baada ya Zimbabwe kupigwa marufuku na Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA).