1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Morocco yachaguliwa rais wa baraza la haki za binadamu 2024

Josephat Charo
10 Januari 2024

Balozi wa Morocco mjini Geneva amechaguliwa kuwa rais wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mwaka 2024 katika kura ya siri ya nadra miongoni mwa nchi wanachama.

https://p.dw.com/p/4b5nL
Uswis | Kikao cha Baraza la haki za Binadamu | Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akihutubia Baraza la Haki za BinadamuPicha: Benoit Doppagne/Belga/dpa/picture alliance

 Omar Zniber ameshinda kura 30 katika kinyang'anyiro na balozi wa Afrika Kusini, Mxolisi Nkos, ambaye amepata kura 17. 

Ilikuwa zamu ya bara la Afrika kuchukua urais wa baraza hilo lakini nchi za Afrika hazikuweza kukubaliana juu ya mgombea mmoja kutoka kwa jumla ya wanachama 13 wa baraza hilo, ndio maana kukafanyika kura ya siri.

Soma pia: EU, AU wakubaliana kuimarisha ushirikiano

Baada ya kushinda, Zniber amesema kazi ya baraza hilo ni muhimu na ni ya msingi: kulinda na kuheshimu haki za binadamu kama zinavyotambulika kimataifa.

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa lilianzishwa mnamo 2006 na lina kazi ya kulinda, kuendeleza haki za binadamu kote ulimwenguni na kushughulikia vitendo vya ukiukaji.

Urais wake huzunguka kila mwaka kati ya makundi matano ya baraza hilo.