Morocco wachaguwa bunge jipya
7 Oktoba 2016Chama cha Haki na Maendeleo (PJD) kinachofuata siasa za Kiislamu kinapambana na wapinzani wa kiliberali, ambao wanadai chama hicho kinataka "kuurudisha nyuma Uislamu" katika jamii ya Morocco.
Licha ya wananchi kuamua nani aingie bungeni, mamlaka kamili yanasalia mikononi mwa Mfalme Mohammed VI, ambaye ni kizazi za utawala wa kifalme uliodumu kwa miaka 350 sasa katika taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.
Katiba mpya iliyopitishwa wakati wimbi la mageuzi likivuma kwenye mataifa ya Kiarabu na kuziangazusha baadhi ya tawala, ilihamisha baadhi ya madaraka ya mfalme kwa bunge.
Hatua hiyo ilisaidia kuinusuru Morocco kwenda njia ya majirani zake wa Tunisia, Misri na Libya.
Serikali ya Waziri Mkuu Abdelilah Benkirane wa PJD inajumuisha pia Wakomunisti, Waliberali na Wahafidhina.
Chama hicho kinapigania muhula wa pili ili kuendeleza mipango yake ya mageuzi ya uchumi na kijamii.