1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Montenegro yapiga kura katika uchaguzi wa bunge

11 Juni 2023

Raia wa Montenegro wanapiga kura leo katika uchaguzi wa bunge unaolenga kumaliza miezi kadhaa ya mkwamo wa kisiasa baada ya serikali kuvunjika Agosti mwaka jana.

https://p.dw.com/p/4SRXg
Montenegro | Parlaments Wahlen
Picha: Europe Now

Uchaguzi huo unafanyika ikiwa ni miezi michache tu baada ya mfumo wa kisiasa wa Montenegro kutikiswa wakati kiongozi wa muda mrefu Milo Djukanovic kushindwa vibaya kabisa katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais mwezi Aprili dhidi ya kiongozi chipukizi Jakov Milatovic, na kumaliza miongo kadhaa ya utawala wa kiongozi huyo.

Uchaguzi wa leo huenda ukatoa taswira ya wapi taifa hilo la Balkan linaelekea wakati likiingia katika enzi mpya ya kisiasa huku nchi hiyo ikiendelea kushikilia lengo lake la kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Chama cha Rais Milatovic cha Europe Now, ambacho kiliundwa mwaka wa 2022 kimepata umaarufu nchini Montenegro kutokana na jukwaa lake la kuunga mkono Ulaya na ahadi ya kuongeza mishahara na kuanzisha mageuzi.

Kitapambana na vyama kadhaa yakiwemo makundi yanayowaunga mkono Waserbia na yanayoegemea Urusi pamoja na cha DPS chake Djukanovic.