1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA:Rauni ya pili ya uchaguzi nchini Liberia

17 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CERD

Mcheza mpira wa zamani anaegombea urais nchini Liberia,George Weah anaongoza katika uchaguzi wa kwanza kupata kufanywa nchini humo tangu kumalizika kwa vita vilivyodumu miaka 14.Juu ya hivyo kuna uwezekano wa kufanywa duru ya pili ya uchaguzi ikikhofiwa kuwa hakuna mgombeaji atakaepata uwingi mkubwa wa kutosha na kujitokeza kama mshindi.Mgombea urais anahitaji kushinda asili mia 51 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi wa Oktoba 11 ili kuzuia duru ya pili.Mkuu wa Halmashauri ya Uchaguzi,Frances Johnson-Morris amearifu mjini Monrovia kuwa George Weah,hadi hivi sasa amejinyukulia asili mia 30 ya kura zilizopigwa,kulinganishwa na asili mia 20 za mpinzani wake mkuu,Ellen Johnson-Sirleaf aliewahi kuwa mtaalamu wa kiuchumi wa Benki Kuu ya Dunia.Duru ya pili ya uchaguzi wa rais inatazamiwa kufanywa mapema mwezi Novemba.