1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA:Rais Obasanjo aelekea Liberia kukutana na kiongozi wa mpito na wagombea

7 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEU6

Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria anaelekea hii leo nchini Liberia kwa mazungumzo na kiongozi wa mpito wa nchi hiyo pamoja na wagombea katika uchaguzi utakaofanyika wiki ijayo.

Rais Obasanjo amekuwa na jukumu muhimu katika kuhakikisha mazungumzo ya amani ya mwaka 2003 yaliyomaliza vita vya waasi na kutoa njia kwa rais wa zamani Charles Tailor kujiuzulu na kuhamia Nigeria.

Kwa mujibu wa redio ya taifa ya Liberia rais Obasanjo atakutana na baadhi ya wagombea 22 wa uchaguzi ujao wa Oktoba 11.

Msemaji war ais Obasanjo nchini Nigeria Remi Oyo amesema madhumuni ya ziara hiyo ni kuonyesha mshikamano war ais ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.