1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Monrovia. Uchaguzi mkuu Liberia umoja wa mataifa waridhia.

12 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CESj

Ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Liberia umesema kuwa umeridhishwa na hali ya usalama ambayo imekuwapo wakati wa uchaguzi mkuu nchini humo.

Waliberia walikwenda kupiga kura jana Jumanne katika uchaguzi wao wa kwanza wa rais na bunge tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo vilivyochukua muda wa miaka 14 miaka miwili iliyopita.

Kutoka kundi la wagombea 22 wa kiti cha urais , wagombea wanaoonekana kupata nafasi za mbele ni pamoja na mwanasoka mashuhuri duniani George Weah.

Baada ya kupiga kura , ameeleza matumaini yake kuhusu matokeo ya uchaguzi huo. Wengine wanaoonekana kuwa katika mstari wa mbele ni pamoja na mwanauchumi ambaye aliwahi kuwa katika benki kuu ya dunia Ellen Johnson- Sirleaf.

Amesema kuwa uchaguzi huo ni ishara ya mabadiliko nchini Liberia. Matokeo ya mwanzo yanatarajiwa baadaye leo.