1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONROVIA: Mikutano ya kuijenga upya Liberia yaanza

5 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFlv
Serikali ya mpito ya Liberia leo hii imeanza mikutano kadhaa ya kutathmini mahitaji ya kuijenga upya nchi hiyo baada ya kipindi cha vita kabla ya kuanza kwa mkutano wa wafadhili uliopangwa kufanyika mjini New York mwezi ujao.

Vita vya miaka 14 vya karibu kila siku vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilioko katika mwambao wa Bahari ya Atlantiki vimemalizika mwezi wa Augusti baada kwenda uhamishoni kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Charles Taylor.

Liberia imekuwa chini ya mamlaka ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa tokea mwezi wa Oktoba katika jitihada za kuhakikisha kunakuwepo kwa amani ya kudumu baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyouwa watu 300,000 na kuwafanya wakimbizi maelfu wengine.