SiasaAsia
Modi kuelekea Moscow
5 Julai 2024Matangazo
Awali ziara hiyo ilitangazwa na maafisa wa Urusi mwezi uliopita lakini hawakuwa wamebainisha tarehe ya kufanyika kwake.
Urusi ina mafungamano mazuri na India tangu enzi za Vita Baridi na umuhimu wa New Delhi kama mshirika mkubwa wa kibiashara umeongezeka tangu kuanza kwa vita vya Ukraine.
Soma zaidi: Rais wa halmashauri kuu EU akutana na waziri mkuu India Narendra Modi
China na India zimekuwa wanunuzi wakubwa wa mafuta ya Urusi kufuatia vikwazo vya Marekani dhidi ya Moscow na washirika wake wa Magharibi.
Chini ya uongozi wa Modi, India imekwepa kuikosowa Urusi kwa uvamizi wake dhidi ya Ukraine, huku ikisisitiza haja ya kupatikana suluhisho kwa njia za amani.