1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Modi afanya mazungumzo ya simu na Putin

16 Desemba 2022

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi leo amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais Vladimir Putin wa Urusi na kurejea wito wake wa kukomeshwa kwa vita nchini Ukraine kwa kutumia njia za kidiplomasia na majadiliano.

https://p.dw.com/p/4L4TO
Wladimir Putin mit Narendra Modi in Samarkand
Picha: Alexandr Demyanchuk/SPUTNIK/AFP

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi leo amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais Vladimir Putin wa Urusi na kurejea wito wake wa kukomeshwa kwa vita nchini Ukraine kwa kutumia njia za kidiplomasia na majadiliano.

 Hayo yameripotiwa na shirika la habari la Reuters likinukuu taarifa zilizotolewa na ofisi ya waziri mkuu Modi na ikulu ya Urusi, Kremlin. Kulingana na taarifa hizo, rais Putin alitumia mazungumzo hayo kumpatia waziri mkuu Modi tathmini ya mzozo nchini Ukraine pamoja na kusifu kuimarika kwa mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

 Modi ambaye nchi yake imejizuia kuchukua upande katika vita nchini Ukraine amekuwa akipigia upatu kumalizika kwa mzozo unaoendelea, na mwezi Septemba alimweleza rais Putin bila kificho kuwa "enzi ya sasa, siyo ya vita"