1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mnangagwa asamehe wafungwa 4,000

19 Aprili 2024

Rais Emmerson Mnangagwa ametoa msahama kwa zaidi ya wafungwa 4,000 ikiwemo baadhi waliokuwa wanasubiri adhabu ya kifo.

https://p.dw.com/p/4ey2j
Emmerson Mnangagwa
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe.Picha: Tsvangirayi Mukwazh/AP Photo/picture alliance

Tangazo la msamaha huo lilitolewa siku ya Alhamisi (Aprili 18), ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za miaka 44 ya uhuru wa nchi hiyo.

Msamaha huo wa rais ambao ni wa pili katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja utawanufaisha wafungwa wanawake, wazee, wenye maradhi yasiyopona na walio na umri mdogo. 

Soma zaidi: Zimbabwe yatangaza Agosti 23 kuwa tarehe ya uchaguzi mkuu

Baadhi ya wafungwa waliohukumiwa kifo lakini hukumu hiyo ikabadilishwa kuwa kifungo cha maisha gerezani nao watanufaika na msamaha huo.

Hata hivyo, kundi hilo litahusisha wale waliokwishatumikia kifungo kwa angalau miaka 20.

Zimbabwe ilipata mwaka 1980 baada ya kufanikiwa kuufikisha mwisho utawala wa wazungu wachache.

Ilibadili jina kutoka Rhodesia na kuanza kuitwa Zimbabwe. 

Taifa hilo la kusini mwa Afrika ni miongoni mwa nchi 50 duniani ambazo bado zinatoa hukumu ya adhabu ya kifo. 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW