1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg nchini Rwanda unapungua

Sylvia Mwehozi
18 Oktoba 2024

Mlipuko wa virusi hatari vya Marburg nchini Rwanda unapungua baada ya chanjo kutolewa kwa watu walio hatarini zaidi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa afya.

https://p.dw.com/p/4lvvt
Kipimo cha kirusi cha Marburg
Daktari akiwa amebeba kipimo cha kirusi cha MarburgPicha: DmitriySk/Depositphotos/IMAGO

Mlipuko wa virusi hatari vya Marburg nchini Rwanda unapungua baada ya chanjo kutolewa kwa watu walio hatarini zaidi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa afya. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa waziri wa afya wa Rwanda Sabin Nsanzimana na Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC. Mapema mwezi Oktoba,Rwanda ilianza kutoa dozi za chanjodhidi ya virusi vya Marburg ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa unaokaribiana na Ebola katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Katika hatua nyingine mkuu wa Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC Jean Kaseya amesema visa vipya vya ugonjwa wa Mpox vinaenea katika nchi nyingine za Afrika. Amesema idadi ya nchi zilizoathiriwa imeongezeka kutoka nchi sita mwezi Aprili hadi 18 mwezi Oktoba.