1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBurundi

Mkuu wa UNHCR ziarani Burundi kuwatembelea wahamiaji wa DRC

10 Februari 2023

Mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, Philippo Grandi, yuko nchini Burundi tangu jana Alhamisi kuzitembelea kambi zinazowahifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4NJoP
Kenia UN Tigray Filippo Grandi
Picha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance

Mkuu huyo wa UNHCR alipokelewa kwa mazungumzo na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye na kujadili kwa kina mzozo wa wakimbizi wa Kongo kwenye kanda ya Maziwa Makuu.

Kwenye mazungumzo Grandi ameahidi kuuhamasisha ulimwengu juu ya umuhimu wa kuiunga mkono Burundi katika suala hilo la wakimbizi.

Pia kiongozi huyo wa shirika la UNHCR amesema amefurahishwa na hatua ya wakimbizi zaidi ya laki 2 wa Burundi ambao tayari wamerejea nchini mwao kutoka nchi za Tanzania, Rwanda, Kongo na Kenya.