1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMexico

Mkuu wa Uhamiaji Mexico kushtakiwa

12 Aprili 2023

Mkuu wa Taasisi ya Kitaifa ya Uhamiaji ya Mexico Franscisco Garduno, atakabiliwa na mashtaka ya uhalifu kuhusiana na kisa cha moto kilichosababisha vifo vya wahamiaji 40 katika mji wa Ciudad Juarez mwezi uliopita.

https://p.dw.com/p/4Pwh1
Waandamanaji nchini Mexico
Mkasa wa moto uliowaua wahamiaji 40 ulizusha maandamano makubwa MexicoPicha: Daniel Cardenas/AA/picture alliance

Waendesha mashtaka wa serikali ya nchi hiyo, wamesema kuwa Garduno, hakuchukuwa hatua za tahadhari licha ya dalili za mapema za matatizo katika vituo vya kuwazuia wahamiaji vya idara yake.

Uamuzi huo wa kumfungulia Garduno mashtaka ulitangazwa jana jioni na ofisi ya mwanasheria mkuu.

Hatua hiyo imefuatia miito ya mara kwa mara kutoka ndani ya Mexico na baadhi ya mataifa ya Amerika ya Kati ya kumchukulia hatua afisa huyo mkuu mbali na maafisa wengine watano, walinzi na mhamiaji mmoja wa Venezuela ambao tayari wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji.