1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa shirika wa misaada ya kiutu awasili Port Sudan

3 Mei 2023

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kiutu na masuala ya dharura, Martin Griffiths amewasili Port Sudan kwa ajili ya kutathmini upelekaji misaada

https://p.dw.com/p/4Qq4P
Schweiz UN l Jemen-Geberkonferenz in Genf l Martin Griffiths
Picha: Fabrice Coffrini/AFP

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kiutu na masuala ya dharura, Martin Griffiths amewasili Sudan kwa ajili ya kujadiliana kuhusu njia za kupeleka misaada kwa raia waliokwama kutokana na mapigano kati ya majenerali wawili hasimu.

Griffiths ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba amewasili katika mji wa Port Sudan ili kuonesha dhamira ya Umoja wa Mataifa kwa watu wa Sudan.

Wakati huo huo, mashambulizi ya anga yamesikika leo katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, wakati ambapo pande hasimu zimekubaliana kusitisha makubaliano kwa siku saba kuanzia kesho Alhamisi.

Umoja wa Mataifa umesema mapigano ya Sudan yamesababisha mzozo wa kibinaadamu, huku watu wapatao 100,000 wakilazimika kukimbilia kwenye nchi jirani huku wakiwa na chakula au maji kidogo.