Mkuu wa NATO asema vita vya Ukraine vitachukua muda mrefu
10 Novemba 2023Matangazo
Lakini ameonya katika mahojiano na shirika la habari la Ujerumani dpa kwamba, mafanikio kamili yatakuwa magumu na yatachukua muda mrefu.
Urusi yazidisha mashambulizi katika mji wa Ukraine wa Avdiivka
Stoltenberg amesema msaada wa kijeshi ndio hatua pekee inayoweza kuhakikisha Ukraine inabaki kuwa nchi huru na ya kidemokrasia, na imshawishi rais wa Urusi Vladimir Putin, kwamba hataweza kushinda kwenye uwanja wa vita.
Vikosi vya Urusi viliivamia Ukraine mnamo Februari, 2022 na hadi sasa imenyakua majimbo manne kusini na mashariki mwa Ukraine, kinyume na sheria ya kimataifa.