Mkuu wa NATO: Ukraine kujiunga na NATO siku moja
20 Aprili 2023Stoltenberg ameahidi kuendelea kiunga mkono nchi hiyo wakati alipozuru Kyiv leo kwa mara ya kwanza tangu uvamizi kamili wa Urusi zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Acha niseseme wazi. Mahali sahihi pa Ukraine ni katika familia ya NATO. Na baada ya muda, uungaji mkono wetu utakusaidieni kutimiza hilo. Hii leo, rais na mimi tumejadili mpango wa msaada kwa miaka mingi. NATO inasimama nanyi leo, kesho na kadiri itakapohitajika, alisema Soltenberg.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alimhimiza Stoltenberg, ambaye amekuwa muhimu katika kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wanachama wa NATO, kuwashinikiza kutoa msaada zaidi zikiwemo ndege za kivita, makombora na vifaru. NATO haina uwepo wake rasmi nchini Ukraine. Kama shirika la nchi 31 wanachama, NATO hutoa tu msaada usio wa silaha kwa serikali ya Ukraine kama vile jenereta, vifaa vya matibabu, mahema, sare za kijeshi na bidhaa nyingine.