1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza: Mkuu wa kundi la watu wanaopinga ufalme aachiwa.

7 Mei 2023

Mkuu wa kundi la watu wanaopinga ufalme nchini Uingereza Graham Smith aliyekamatwa kabla ya kundi lake kufanya maandamano wakati wa hafla ya kuvikwa taji Mfalme Charles wa tatu, ameachiwa huru.

https://p.dw.com/p/4R0Sb
London | Anti-Monarchie-Demonstranten bei der Krönungsprozession
Picha: Scott Garfitt/AP/picture alliance

Mkuu wa kundi la watu wanaopinga ufalme nchini Uingereza Graham Smith aliyekamatwa Jumamosi kabla ya kundi lake kufanya maandamano wakati wa hafla ya kuvikwa taji Mfalme Charles wa tatu, ameachiwa huru. Kundi hilo linaloitwa Republic, ambalo linataka mkuu wa nchi ya Uingereza aliyechaguliwa, limesema mtendaji Smith aliachiwa, baada ya kuzuiwa kwa saa 16. Polisi wa mjini London wamekosolewa kwa kuwakamata wanachama wa kundi hilo hapo jana. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamefananisha kukamatwa kwa watu hao na matukio kama hayo katika mataifa ambayo polisi wana mamlaka makubwa lakini polisi nchini Uingereza imetetea hatua zilizochukuliwa na maafisa wake na imesema hatua dhidi ya waandamanaji hao zilichukuliwa kulingana na sheria baada ya umma kuelezea wasiwasi wao.