Mkuu wa Kanisa Katoliki Kongo ahimiza utulivu
25 Desemba 2023Matangazo
Ametoa wito huo usiku wa kuamkia leo wakati wa Misa yake ya Krismasi.
Ameongeza kuwa wengi walijitokeza kwa shauku na kwa dhamira ya kufanya maamuzi ya kidemokrasia, lakini kile ambacho kilipaswa kuwa sherehe kubwa ya maadili ya kidemokrasia, kiligeuka kuwa fadhaa kwa wengi.
Soma pia: Kanisa Katoliki Kongo lamshutumu Tshisekedi
Ucheleweshaji mkubwa wa vifaa na matatizo ya hapa na pale yaliathiri uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumatano iliyopita katika baadhi ya vituo.
Wagombea watano wa urais kutoka upinzani, akiwemo Moise Katumbi, wametaka uchaguzi huo ubatilishwe na kufanywa upya, wakisema ulikumbwa na "udanganyifu mkubwa".