MigogoroSudan
Al-Burhan asema hatoshiriki mazungumzo ya amani Uswisi
26 Agosti 2024Matangazo
Al-Burhan badala yake ameapa kuendelea kupigana hata kwa muda wa miaka 100.
Mkuu huyo wa jeshi la Sudan ambaye vikosi vyake vimekuwa vikipambana na wanamgambo wa RSF kwa zaidi ya miezi 16, amewaambia waandishi wa habari mjini Port Sudan kuwa hawatokwenda Geneva kwa ajili ya kushiriki mazungumzo ya amani.
Soma pia: Sudan yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu
Marekani ilianzisha mazungumzo nchini Uswisi mnamo Agosti 14 yaliyolenga kupunguza mateso wanayopitia raia wa Sudan na kufanikisha kusitishwa kwa mapigano.
Licha ya RSF kushiriki kwenye mazungumzo hayo, jeshi la Sudan linaripotiwa kutoridishwa na muundo wa mazungumzo hayo na likaamua kususia, ingawa limekuwa likifanya mazungumzo kwa njia ya simu na wapatanishi.