1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa jeshi la Israel Meja Jenerali Herzi Halevi ajiuzulu

21 Januari 2025

Mkuu wa jeshi la Israel Meja jenerali Herzi Halevi amejiuzulu, kutokana na kushindwa kwenye jukumu lake, wakati wa uvamizi wa kundi la wanamgambo la Kipalestina la Hamas, uliofanyika Oktoba 7 mwaka 2023.

https://p.dw.com/p/4pROu
Herzi Halevi
Mkuu wa jeshi la Israel Meja jenerali Herzi HaleviPicha: Israeli Defense Forces/IDF/dpa/picture alliance

Katika barua ya kujiuzulu kwake ametowa ufafanuzi juu ya sababu za kujiuzulu kwake akikiri kushindwa kwake kuzuia uvamizi wa Oktoba 7 na kusema kwamba anaondoka katika wakati ambapo yamepatikana mafanikio katika jeshi hilo la Israel.

Aidha kiongozi wa upinzani wa Israek Yair Lapid ameitaka serikali ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu ijiuzulu baada ya Halevi kujiuzulu.

Baraza la mawaziri la Israel laidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano.

Wakati huohuo Israel imeanzisha operesheni kubwa ya kijeshi katika mji unaokaliwa kwa mabavu na nchi hiyo wa Jenin,katika Ukingo wa Magharibi.Wizara ya afya ya Palestina imesema takriban watu sita wameuwawa na 35 wamejeruhiwa.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW