Mkuu mpya wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya azuru Kyiv leo
1 Desemba 2024Matangazo
Akizungumza na vyombo vya habari,Costaamesema wamewasili nchini humo kwa kubainisha ujumbe wa wazi kwamba wapo pamoja na Ukraine na wataendelea kuiunga mkono kwa dhati. Wakati ziara hiyo ikifanyika kiongozi wa kijeshi wa mji huo, Serhiy Popko amesema usiku wa kuamkia leo Urusi imefanya mashambulizi kwa kutumia droni katika viunga vya mji wa Kyiv. Hata hivyo hakujawa na taarifa za majeruhi. Katika kipindi cha takriban miaka mitatu ya vita vyake, Urusi mara kwa mara imekuwa ikifyatua makombora na droni katika maeneo ya makazi ya watu, mbali na maeneo ya mapambano, ikilenga haswa maeneo ya uzalishaji wa nishati katika kipindi hiki cha msimu wa baridi.