Mkutano wa uchumi wa dunia waanza mjini Davos
17 Januari 2023Baada ya hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na mwanzilishi wa jukwaa hilo, Klaus Schwab, macho na masikio vinaelekezwa kwenye hotoba ya Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, wakati Ulaya ikikabiliwa na mkururo wa changamoto zikiwemo athari za uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, na machungu yatokanayo mfumuko wa bei na ukuaji hafifu wa uchumi.
Soma pia: Pengo la usawa wa uchumi kijinsia kuzibwa baada ya miaka 257
Mke wa Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine, Olena Zelenska, ni miongoni mwa watu wengine watakaolihutubia jukwaa hilo. Katika ripoti yake ya mwaka juu ya hali ya uchumi wa dunia, Jukwaa la Dunia la Uchumi limesema kupanda kwa gharama ya maisha na mizozo ya nishati na chakula ndivyo vizingiti vikuu kwa wakati huu.