Mkutano wa nchi za kiarabu kuhusu Syria kufanyika Jordan
30 Aprili 2023Viongozi hao watajadili pia juu ya hatua ya kusitisha kuitenga Syria kidiplomasia. Rais wa Syria Bashar al Assad amekuwa akitengwa kisiasa, tangu kuanza kwa mgogoro nchini humo mwaka 2011.
Mnamo wiki za hivi karibuni pamekuwapo juhudi kadhaa za kidiplomasia baada ya Saudi Arabia na Iran, ambaye ni mshirika mkuu wa Syria kurejesha tena uhusiano wa kidiplomasia na Syria.
Soma pia: Mataifa ya Kiarabu yaujadili mgogoro wa Syria
Mawaziri hao watatathmini mawasiliano ambayo yamekwishafanyika baina ya nchi zao na serikali ya Syria kwa lengo la kuleta suluhisho katika mgogoro wa Syria. Mawaziri wa mambo ya nje watakaohudhuria mkutano huo wa mjini Amman wanatoka nchi za Misri, Iraq, Jordan, Saudi Arabia na Syria.
Hata hivyo Qatar ambayo imekuwa inawaunga mkono waasi wa Syria imesema wazo la kuirudisha Syria katika umoja wa nchi za kiarabu halijakuwa thabiti.