SiasaAfrika Kusini
Mkutano wa kilele wa kundi la BRICS waingia siku ya pili
23 Agosti 2023Matangazo
Katika siku ya kwanza ya mkutano huo unaofanyika mjini Johannesburg, Afrika Kusini, viongozi wa mataifa hayo ya Brazil, China, India, Afrika Kusini na Urusi, walitoa hotuba zilizomulika mwelekeo wa kundi hilo la kiuchumi na nafasi yake katika ulimwengu wa sasa.
Rais Vladimir Putin wa Urusi ambaye alihutubia jukwaa hilo kwa njia ya mtandao, alisema kundi hilo limepiga hatua katika utekelezaji wa dhamira yake ya kuachana na utegemezi wa dola ya Marekani katika biashara na uchumi.
Hotuba za viongozi wengine ikiwemo rais Xi Jinping wa China, ziligusia umuhimu wa kuimarisha nafasi ya kundi la BRICS kwenye Jukwaa la Kimataifa.