1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiGhana

kuwepo mfumo wa kuwafidia waliotumika kama watumwa Ghana

17 Novemba 2023

Wajumbe wa mkutano wa kilele wa ulipaji fidia wamekubaliana kuanzisha mfuko wa Kimataifa, kushinikiza ulipaji fidia kwa mamilioni ya Waafrika waliofungwa jela karne zilizopita wakati wa enzi za biashara ya Utumwa, Ghana.

https://p.dw.com/p/4Z2V1
Ghana | Utumwa
Pingu na minyororo iliyotumika wakati wa ukoloniPicha: Russell Contreras/AP Photo/picture alliance

Mkutano huo mjini Accra unaongeza mkazo kwenye miito inayoongezeka ya fidia baada ya Waafrika wapatao milioni 12 kuchukuliwa kwa nguvu na kupelekwa Mataifa ya Ulaya kutumikishwa kama watumwa kati ya karne ya 16 hadi 19 

Karne nyingi baada ya kumalizika kwa biashara ya utumwa, watu wenye asili ya Kiafrika ulimwenguni, wameendelea kuwa waathiriwa wa ubaguzi wa rangi wa kimfumo pamoja na kukumbwa na mashambulizi ya ubaguzi.

Ziara ya Scholz Afrika na shauku ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi

Hayo ni kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya kongamano maalum la Umoja wa Mataifa ambalo liliunga mkono fidia kama kile walichokiita "jiwe la msingi la haki katika karne ya 21."

Amr Aljowailey, balozi na pia mshauri wa naibu mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika aliyeyasoma maazimio ya mkutano huo amesema fidia inategemea kile alichokiita msingi wa haki za kimaadili na kisheria na utu wa watu.