1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa haki za binadamu wa UN wafanyika Geneva

Hawa Bihoga
27 Februari 2023

Zaidi ya wakuu wa nchi na mawaziri 100 watashiriki kikao cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, kujadili mengi ikiwemo madai ya uhalifu wa kivita wa Urusi nchini Ukraine

https://p.dw.com/p/4O16X
Schweiz, Genf | António Guterres im UN-Menschenrechtsrat
Picha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/picture alliance

Wakati wa mkutano huo mataifa yalio mengi yatajaribu kuongezea muda chombo cha uchunguzi cha Umoja wa Mataifa kilichoundwa kuchunguza ukatili nchini Ukraine.

Balozi wa kudumu wa Ukraine katika Umoja wa Mataifa Yevheniia Filipenko amesema ulimwengu utamulika uhalifu wa Urusi nchini Ukraine.

Viongozi duniani wazungumzia mwaka mmoja wa vita Ukraine
"Ni muhimu kwamba watu wa Ukraine wajue kuwa ulimwengu unawakumbuka, kwamba ulimwengu utazungumza juu ya ukatili wa Urusi, uhalifu wa kivita wa Urusi na uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanywa nchini Ukraine," alisema Yevheniia Filipenko.

Kyiv, ambayo imetaka kuanzishwa kwa mahakama maalum ya kuwashtaki uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Urusi juu ya uvamizi huo, imesema chombo hicho kilikuwa muhimu ili kuhakikisha Urusi inawajibika kwa uhalifu wake.

Mara zote Moscow imekuwa ikikanusha juu ya shutuma hizo.