1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Mkutano wa G20 nchini India kukamilika bila tamko la pamoja

18 Julai 2023

Mazungumzo ya siku mbili kati ya mawaziri wa fedha wa kundi la G20, yatakamilika leo Jumanne bila ya kuwa na tamko la pamoja kutokana na kuwepo kwa tofauti kati ya mataifa makubwa kuhusu vita vya nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4U3VL

Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa India ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema, nchi nyingi za magharibi zikiwemo Marekani, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa zilishinikiza kutolewa kwa tamko la pamoja la kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, wakati Urusi na mshirika wake wa karibu China wamepinga hatua hiyo.

Mapema wiki hii waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen alisema moja ya malengo yake mwaka huu ni kupambana na juhudi za Urusi kukwepa vikwazo.