1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Mkosoaji wa Kagame atangaza ari ya kugombea urais

8 Mei 2024

Mkosoaji wa Rais Paul Kagame wa Rwanda, Diane Rwigara, ametangaza leo kuwa anapanga kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4fdaF
Mwanasiasa wa Rwanda Diane Rwigara
Kiongozi huyo wa vuguvugu la People Salvation, alizuiwa kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2017Picha: Getty Images/AFP/C. Ndegeya

Rwigara ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, zamani ukijulikana kama Twitter, kwamba sura mpya ya Rwanda sasa inaanza na kwa pamoja, wataweka historia.

Soma pia: Rwanda inafanya uchaguzi wake mkuu mwezi Julai mwaka huu

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 42, ambaye ni kiongozi wa vuguvugu la People Salvation, alinuwia kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2017 dhidi ya Rwanda lakini akazuiwa.

Soma pia: Victoire Ingabire azuwiliwa kugombea urais Rwanda

Siku chache tu baada ya kutangaza kuwania urais, picha za uchi zinazodaiwa kuwa za Rwigara zilisambaa mtandaoni, ila aliliambia shirika la habari la Marekani la CNN kwamba picha hizo zilibadilishwa kwa lengo la "kumnyamazisha."

Rwanda, ambayo imekuwa ikitawaliwa na Rais Kagame tangu mwisho wa mauaji ya halaiki ya mwaka 1994, inatarajiwa kufanya uchaguzi wa urais na ubunge mnamo Julai 15.