1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mke wa zamani wa aliyekuwa rais wa Liberia asema kushtakiwa kwa Taylor kutafichua siri nyingi

Dinah Gahamanyi13 Januari 2006

Mke wa zamani wa aliyekuwa raisi wa Liberia Charles Taylor bi Jewel Howard Taylor amesema ikiwa bwana taylor atapelekwa mbele ya mahakama ya kimataifa inayoshughulilia makosa ya uharifu wa kivita nchini Sierra Leone siri nyingi zitafichuliwa juu ya uharifu wa kivita nchini humo.

https://p.dw.com/p/CBJK
Rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor
Rais wa zamani wa Liberia, Charles TaylorPicha: AP

Mke huyo wa zamani wa Charles Taylor bi Jewel Howard Taylor aliliambia shirika la habari la AFP kwamba Ikiwa Charles Taylor atapelekwa mahakamani, kwa mtizamo wake watapatikana akina Taylor wengine watakaotakiwa kwenda mbele ya mahakama hiyo .

Alisema hadhani kama hivi sasa Sierra leone imejiandaa kikamilifu kufanya msako mkali kwa kile kwani alisema wapo watu wengi wanaohusika.

’’Kuna hadithi inayosema ukivuta vitu viwili vilivyofungwa kwa kitanzi kimoja msituni vitu vingine pia vitavutwa’’. Alisema bi Haward Taylor .

Bwana Charles Taylor amekuwa akishutumiwa na mahakama ya kimataifa ya uharifu wa kivita nchini Sierra Leone kwamba alikuwa mdhamini wa waasi wa nchini humo walioendesha mashambulizi ya kivita nchini humo kwa miaka takriban 10.-

Bwana Taylor ambaye ni mpiganaji wa zamani ambaye baadae alikuwa raisi ,aliachia madaraka ya kiti cha uraisi wa Liberia August 2003 ili kuruhusu utekelezaji wa wa mpango wa amani wa umoja wa mataifa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka 14.

Taylor amekuwa akiishi katika nyumba ya kifahari, ikiwa na ulinzi mkali katika mji wa kusini mashariki mwa Liberia wa Calabar.Raisi wa Nigeria Olusegun Obasanjo amekuwa akikataa shinikizo kutoka mataifa mbali mbali duniani wakimtaka amkabidhi bwana Taylor katika mahakama hiyo.Raisi Obasanjo amekuwa akisisitiza kuwa atamkabidhi tu kwa watawala waliochaguliwa nchini humo.

Raisi mpya wa Liberia Hellen Johnson Sir Leaf amekwishasema hana haraka ya kulishughulikia swala la Taylor.

Mke wa zamani wa Charles Taylor anasema Watu wengi nchini Liberia watabainika kuhusika na machafuko yaliyoikumba nchi hiyo iliopo Magharibi mwa Afrika. “ Migogoro katika nchi hii haikuanza mwaka 1989,ilianza hata kabla.Ni kizazi kipi kitakachoadhibiwa’’.Alihoji bi Howard Taylor, na kuongeza kuwa wakati huu Sierra leone haina budi kuangalia mambo muhimu ili kuliwezesha taifa kuendelea ,na si kurudi nyuma lilipotoka .

Mke huyo wa zamani wa bibi Charles Taylor ni mwanachama wa Chama cha National Patriotic (NPP) na alichaguliwa kama mjumbe wa baraza la Seneti akiliwakilisha jimbo la Bong lililopo kati kati mwa nchi ya liberia, ambako wakati mmoja iliwahi kuwa ngome ya charles taylor wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Bi Howard Taylor na wabunge wengine watatu waliochaguliwa mwaka jana waliwekewa vikwazo na Umoja wa mataifa kutokana na kwamba ni washirika wa karibu sana wa bwana Taylor.

Licha ya kwamba Rais mpya wa Liberia bi Hellen Johnson Sirleaf alikuwa mpinzani mkubwa wa Taylor alikubali uungaji mkono wa Bi Howard Taylor katika uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka uliopita ,ambapo alipata kura nyingi za wapiganaji wa zamani.

Wakati hayo yakiarifiwa mke wa raisi wa Marekani George W Bushi bi laura Bush ,na waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Condoleeza Rice, wanaelekea mjini Monlovia nchini Liberia kwa ajili ya kushiriki sherehe za kuapishwa kwa bi Johnson Sir Leaf jumatatu ijayo. Ziara hiyo inalenga kuonyesha uungaji mkono wa Marekani kwa viongozi wa kiafrika.

Dinah Gahamanyi