Mke wa Sanchez atoa ushahidi wa rushwa kwenye biashara zake
5 Julai 2024Kesi hiyo ya ufisadi kwa kiasi kikubwa ilimkasirisha waziri mkuu Sanchez.
Mahakama ya mjini Madrid mwezi uliopita ilimtaka Gomez atoe ushahidi leo Julai 5 kama mtu anayechunguzwa katika uchunguzi huo wa mahakama kuhusiana na tuhuma za ufisadi katika sekta ya binfasi pamoja na ushawishi wa kisiasa.
Kambi ya upinzani ya chama cha mrengo wa kulia imekuwa ikilipalilia suala hili kama ushahidi wao wa tuhuma wanazotowa, kwamba waziri mkuu Sanchez na serikali yake ni mafisadi.
Uchunguzi wa awali ulianzishwa Aprili 16 kufuatia kesi ya malalamiko iliyofunguliwa na shirika moja lisilokuwa la kiserikali la kupambana na rushwa linaloitwa Manos Limpias ambalo linafungamanishwa na chama cha siasa kali.
Kesi hiyo imemuweka katika hali ngumu waziri mkuu Sanchez ambaye mwishoni mwa mwezi Aprili alitangaza kufikiria kujiuzulu kufuatia kile alichokiita kampeni ya kumdhalilisha kisiasa inayofanywa na vyama vya mrengo wa kulia.