Mke wa mshindi wa tuzo ya Nobel ya amani awekwa kizuizini
11 Oktoba 2010Matangazo
Msemaji wa Shirika la haki za binadamu la Marekani lenye makaazi yake nchini China, amesema Bibi Liu Xia amewekwa katika kizuizi cha nyumbani.
Alikuwa amekwenda kumtembelea mume wake gerezani ili kumpa habari za ushindi wa tuzo ya amani na kwamba aliporudi nyumbani kwake mjini Beijing alizuiwa asitoke.
Liu Xiaobo alishinda tuzo ya amani ya Nobel siku ya Ijumaa kutokana na miongo miwili ya harakati zake zisizotumia nguvu ili kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinaheshimiwa nchini China.
Mwandishi: Halima Nyanza(ZPR)
Mhariri: Sekione Kitojo