Mkataba wa Geneva unafanyakazi kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadamu.
8 Juni 2007Mkataba huo unabaki kuwa muhimu katika kuwalinda raia katika maeneo ya mizozo na kurekebisha zaidi jinsi ya uendeshaji wa vita. Picha hizi zinaonyesha madhila ya kiutu katika mizozo ya kivita. Pia zinatukumbusha kuwa, hata wakati wa vita, hii ndio mipaka, amesema Pauline Wall kutoka katika shirika la kimataifa la msalaba mwekundu, ICRC.
Iwapo vita vilikuwa vigumu kueleweka katika mwaka 1977, imekuwa vigumu zaidi katika mwaka 2007. Mapambano ya silaha yamekuwa hivi sasa aghalabu kati ya taifa na taifa , lakini mara nyingi ni suala la ndani, linalowahusisha makundi tofauti. Raia mara nyingi ndio wanaoangukia kuwa wahanga wa vita, wakiwakilisha karibu asilimia 90 ya wahanga katika mizozo inayotokea hivi sasa. Pamoja na kujikuta katika mapigano na kuwa kama kile kinachojulikana kama uharibifu ziada, lakini mara nyingi wanalengwa maksudi, kama inavyotokea nchini Iraq na Afghanistan.
Mara nyingi wale wanaobeba silaha hawaheshimu sheria za kimataifa za kiutu. Picha hizi zilichochukuliwa na wapigapicha wataalamu, pamoja na wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu , zinaleta uhalisi wa unyama ambao mapambano ya silaha yanaendelea kuathiri raia.
Raia wanakumbana na matumizi ya nguvu, kupoteza nyumba zao pamoja na kupotezana wanafamilia baada ya kukimbia huku na huko kusalimisha maisha yao, na wanakosa chakula, maji na huduma za utatibabu, anasema Jean-Luc Metzker, mkuu wa ujumbe wa kimkoa wa shirika la msalaba mwekundu katika eneo la Pacific.
Nyongeza ya mwaka 1977 katika mkataba huo , ambayo inasema kuwa mkataba wa mwaka 1949 wa Geneva , umekuwapo kutokana na kubadilika kwa sura ya mapambano, hususan kuzuka kwa vita vya msituni pamoja na maendeleo ya kiufundi katika teknolojia ya silaha. Kupanuka kwa uwanja wa vita hadi kwa raia kunaleta hatari kubwa , na mkataba umeimarisha ulinzi wa wahanga wa mapambano hayo ya silaha. Nyongeza ya kipengee nambari mbili kwa mara ya kwanza imeongeza ulinzi kwa raia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Wakati mkataba huo unakubalika duniani kote, dunia lakini imejaa mifano kadha ya sheria kuendewa kinyume katika mizozo ya leo iwe ni Iraq, Afghanistan , Sudan ama Colombia ama Rwanda na katika maeneo ya Balkan. Kampeni za kigaidi dhidi ya raia na vitendo vya ubakaji, uandikishaji wa wapiganaji watoto , kuwalazimisha watu kukimbia makaazi yao, hayo yote yamekuwa ni mazoea katika wakati huu.