1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Volker Perthes ajiuzulu kuushughulikia mgogoro wa Sudan

14 Septemba 2023

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia maswala ya Sudan Volker Perthes, amejiuzulu. Perthes alitangaza kujiuzulu kwake alipolihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/4WK0j
USA UN l Sonderbeauftragter des Generalsekretärs der Vereinten Nationen für Sudan,  Volker Perthes
Picha: Eskinder Debebe/UN/Xinhua/IMAGO

Mjumbe huyo maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia maswala ya  Sudan katika hotuba yake ya mwisho kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, alionya kwamba mzozo kati ya viongozi wa kijeshi wa Sudan unaweza kubadilika na kuwa vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hiyo inayokabiliwa na mapigano kwa sasa kati ya majenerali wawili wanaogombea nafasi.

Volker Perthes, aliyejiuzulu kama mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa wa maswala ya Sudan.
Volker Perthes, aliyejiuzulu kama mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa wa maswala ya Sudan. Picha: Derek French/IMAGO

Mjumbe huyo maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Sudan aliyejiuzulu amesema mzozo wa Sudan unaweka historia mbaya ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Amesisitiza kuwa mashambulizi ya kiholela dhidi ya raia yanayofanywa na pande zinazopigana ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

Soma:MSF:Mashambulizi ya raia yamefikia kiwango cha kutisha Sudan

Ameeleza kuwa takriban watu 5,000 wameuawa tangu mapigano yalipoanza nchini Sudan na zaidi ya watu 12,000 wamejeruhiwa, na kwamba idadi hizo zinaweza kuwa kubwa zaidi.

Wajumbe katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Wajumbe katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Picha: Manuel Elias/Xinhua/IMAGO

Mjumbe huyo amezungumzia juu ya kuwepo makaburi 13 ya halaiki ndani na karibu ya mji mkuu wa jimbo la Darfur Magharibi, Geneina kulingana na ripoti ya kuaminika ya Ofisi ya Pamoja ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa aliyopokea.

Wakati hayo yakijiri takriban raia 40 waliuawa katika shambulio la anga katika eneo la magharibi mwa Sudan, Darfur hapo jana Jumatano wakati mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan alipoielekea nchini Uturuki.

Kiongozi wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan
Kiongozi wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al-BurhanPicha: Sudanese Army/AFP

Ziara ya Burhan nchini Uturuki ni safari yake ya tano nje ya nchi tangu mwishoni mwa mwezi Agosti akitafuta kuungwa mkono katika mvutano mkubwa wa madaraka na naibu wake wa zamani Mohammed Hamdan Daglo.

Vyanzo: DPA/AFP/AP