1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mjumbe wa Baraza la Vita Israel akutana na maafisa Marekani

4 Machi 2024

Benny Gantz, mjumbe wa Baraza la Vita la Israel amefanya ziara nchini Marekani na kukutana na maafisa wa serikali licha ya kutokubaliwa kufanya hivyo na Waziri Mkuu wake Benjamin Netanyahu.

https://p.dw.com/p/4d9ws
Benny Gantz na Antony Blinken
Waziri wa Mambo wa Marekani Antony Blinken akiwa katika mazungumzo na Benny Gantz.Picha: Chuck Kennedy/U.S State Department/abaca/picture alliance

Mjumbe wa juu wa baraza linalosimamia vita nchini Israel, Benny Gantz, anakutana na maafisa waandamizi wa serikali ya Marekani mjini Washington wakati mazungumzo yanaendelea nchini Misri ili kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza kabla ya kuanza mwezi mtukufu kwa Waislamu wa Ramadhan wiki ijayo.

Soma pia:Mafanikio makubwa yaripotiwa katika vita vya Gaza 

Afisa mmoja kutoka kwenye chama cha Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu cha mrengo wa kulia cha Likud amesema Gantz, ambaye ni mpinzani mkubwa wa kisiasa wa Netanyahu, alisafiri bila ya idhini ya waziri wake mkuu.

Ama katika mazungumzo ya nchini Misri juu ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, Israel haikupeleka wajumbe mjini Cairo kwa sababu inasubiri majibu kutoka kwa Hamas kuhusu maswali mawili, kulingana na maafisa wa Israel.