1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjadala wa hoja ya ukandamizwaji wa demokrsia Tanzania

23 Novemba 2020

Nchini Tanzania kuna mjadala mkubwa unaendelea hasa baada ya Waziri wa Mambo ya nje kutoa kauli inayokosa mataifa ya magharibi, akisema Tanzania haitakuwa tayari kupokea misaa yenye masharti yanayodhalilisha utu wake.

https://p.dw.com/p/3lhzT
Tansania Amtseid des Präsidenten John Pombe Magufuli
Picha: Tanzania Presidential Press Service

Kauli ya waziri Palamagamba Kubudi mwishoni mwa wiki inakuja baada ya baadhi ya wabunge wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kuhoji namna ukandamizwaji wa demokrasia, mwenendo wa uchaguzi mkuu na msaada uliotolewa na jumuhia hiyo kuhusu janga la Corona.

Wengi wanaona kauli ya waziri huyo imekwenda mbali zaidi na hata kuweza kuzorotesha uhusiano wa diplomasia na mataifa mengine, ingawa wengine wakisifia wakiieleza kwamba Tanzania ni taifa huru hivyo lina mamlaka ya kujiendeshewa mambo yake pasi na kuingiliwa na dola yoyote ya nje.

Baadhi ya watoa maoni wanahisi Tanzania inahitajia zaidi kusaka maelewano

Baadhi ya wachambuzi wanasema Waziri Kabudi angeweza kufikisha ujumbe wake kwa wale waliolenga kwa kutumia lugha ya kidiplomasia na yenye kutaka kusaka maelewano jambo ambalo pia limeungwa mkono na baadhi ya wanasiasa.

Wachambuzi wengi walioitupia jicho kali ya Waziri Kabudi ambaye ni moja ya mawaziri wawili tu walioteuliwa hivi karibuni tangu serikali ya awamu ya tano ianze ungwe ya pili ya utawala wake, wanasema inafaa kujadiliwa kwa mapana.

Onyo kutoka kwa upande wa wanasiasa

Mwanasiasa wa siku nyingi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Sammy Ruhuza anaona kuwa kitendo cha waziri Kabudi kuzikosoa waziwazi kinaweza kuzusha mjadala mwingine mkubwa katika duru za kimataifa. Hata hivyo, kwa upande mwingine wapo wanaoiona kauli ya Waziri huyo kama kielelezo tosha kinachojaribu kutafsiri utashi wa taifa linalotaka kutoingiliwa kwa baadhi ya masuala yake ya ndani.

Tansania | Mitglied der NCCR-Mageuzi-Partei | Konferenz
Wajumbe wa chama cha NCCR MageuziPicha: DW/S. Khamis

Wanasema kama ilivyo kwa baadhi ya madola makubwa ambayo yamekuwa yakiweka misingi yake ya kupinga kuajdiliwa baadhi ya masuala yake ndivyo inapaswa kuchukuliwa kwa mataifa hata yale machanga. Wakati akizungumza kwa mara ya kwanza tanguapishwa kwenye wadhifa wake, Waziri Kabudi alionyesha kukerwa namna masharti magumu yanavyotolewa kwa Tanzania wakati inapokuja suala la upokeaji wa misaada.

Soma zaidi:Tanzania: Ukandamizaji ulihujumu uchaguzi

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoko kusini mwa jangwa la sahara ambayo pamoja na kutegemea fedha zake za ndani kuendesha miradi mingi lakini imekuwa ikipokea kiasi kikubwa cha fedha kwa mwaka kutoka kwa wahisani wa nje kwa ajili ya kugharimia miradi mbalimbali.

Chanzo: DW