1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mizozo na Utatuzi - Palipo na Wazee

14 Agosti 2013

Hata katika karne ya 21, migogoro inaonekana kuwa jambo lisiloepukika duniani kote. Migogoro inaweza kusuluhishwa kwa njia ya amani kwa sababu ya utamaduni wa Kiafrika wenye mbinu nyingi za kutafuta suluhu.

https://p.dw.com/p/19OWX
Vijana wawili wanapeana mikono (Picha: Frank May/ pa)
Picha: picture-alliance / Frank May

Ninawezaje kushinda katika hali ya mgogoro? Hili ni swali linalowasumbua wasikilizaji wengi vijana wa Deutsche Welle. Baadhi yenu mlikuja kwa watu wa Learning by Ear na kushauri tutengeneze kipindi kuhusu mada hii. Kwa sababu ingawa vijana wengi wa Kiafrika wanaishi katika nchi zenye amani, baadhi yao bado wanateseka na vita.

Mchezo huu wa redio unalenga kutafuta njia za kutatua migogoro bila kutumia nguvu. Tutakutana na Masambo na Mitumba, wakuu wawili wa familia wenye makabila tofauti na wanaoishi pamoja katika bonde lenye rutuba liitwalo Kijani. Masambo na Mitumba wana mizozo mbali mbali. Je, wataweza kupata suluhu ya kudumu na kuishi kwa amani? Mfululizo huu utawasaidia wasikilizaji kufahamu mbinu za kutatua migogoro katika maisha yao.

Vipindi vya Deutsche Welle Noa Bongo! Jenga Maisha Yako vinapatikana katika lugha sita: Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kihausa, Kireno na Kiamhara.