Misri yaandaa mkutano kuyakutanisha makundi ya kisiasa Sudan
29 Mei 2024Matangazo
Hayo yameelezwa jana na wizara ya mambo ya kigeni ya nchi hiyo. Mkutano huo unalenga kutafuta makubaliano kati ya makundi ya kiraia ya Sudan kuhusu njia za kujenga amani thabiti na ya kudumu.
Watu 85 wauwawa kufuatia mapigano makali Sudan
Mpaka sasa mataifa ya kikanda na kimataifa ikiwemo Marekani, Misri na Saudi Arabia yamejaribu kutafuta makubaliano ya amani kati ya pande zinazopigana,bila ya mafanikio.
Tangu mwaka 2023 Sudan iko kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi la serikali likiongozwa na jenerali Abdel Fattah al-Burhan na kundi la wanamgambo la RSF linaloongozwa na Hamdan Dagalo.Maelfu ya raia wanakadiriwa kuuwawa.