Misri kupokea mkopo wa dola bilioni 1.2 kutoka IMF
6 Januari 2025Matangazo
Waziri wa Fedha wa Misri, Ahmed Koushouk, alisema kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni hapo jana kwamba kikao cha ngazi za juu cha IMF kinachokaa mwezi huu wa Januari kitaipatia nchi yake mkopo huo, kama sehemu ya programu itakayochukuwa hadi mwezi Machi.
Soma zaidi: Misri yafanya mkutano wa kilele wa nchi za Kiislamu
Kuporomoka kwa mapato yatokanayo na Mfereji wa Suez kulikochochewa na vita kwenye Ukanda wa Gaza kumeifanya Misri kukabiliwa na uhaba wa fedha za kigeni na kupanda kwa gharama za maisha. Misri inategemea mikopo na ufadhili wa kimataifa kujikwamuwa kwenye mkwamo wake wa kiuchumi.