1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri kupiga marufuku makundi ya haki za binaadamu

Sekione Kitojo
31 Mei 2017

Shirika la haki za binaadamu la Amnesty International linasema sheria mpya iliyoidhinishwa na Rais Abdel Fattah Al-Sisi wa Misri kuzidhibiti asasi za kiraia ni 'hukumu ya kifo' kwa makundi ya haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/2dvBe
Abdel-Fattah al-Sissi
Picha: picture-alliance/dpa

Katika taarifa yake, shirika hilo limeiita sheria hiyo iliyotiwa saini na Rais Sisi hapo jana, kuwa ni pigo la maafa kwa makundi ya haki za binadamu yanayofanyakazi nchini Misri. 

Ukali wa vizuwizi vilivyowekwa na sheria hiyo unatishia kuziuwa asasi hizo katika wakati ambapo maafisa wakiendeleza ukandamizaji dhidi ya upinzani wanafanya kazi zao kuwa muhimu sana kuliko wakati mwingine wowote, amesema Najia Bounaim, mkurugenzi wa kampeni wa shirika hilo katika mataifa ya Afrika Kaskazini.