SiasaMisri
Misri kufanya uchaguzi wa urais Desemba 2023
25 Septemba 2023Matangazo
Rais wa nchi hiyo Abdel Fattah al-Sisi, kwa kiasi kikubwa anatarajiwa kushinda uchaguzi huo, licha ya kukabiliwa na mgogoro wa kiuchumi ikiwa ni pamoja na mfumuko wa bei na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni.
Al-Sisi, 68, ataweza kugombea muhula wa tatu kufuatia marekebisho ya katiba ya mwaka 2019, ambayo pia yameongeza muda wa muhula wa rais kutoka miaka miaka minne hadi sita, na hilo huenda likamuwezesha kusalia madarakani hadi angalau mwaka 2030.
Tume inayosimamia uchaguzi nchini Misri imesema matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa Desemba 23 na, ikiwa kutakuwepo duru ya pili, matokeo ya mwisho yanapaswa kutangazwa Januari 16.