Milipuko yatokea katika kambi ya UN nchini Mali
6 Desemba 2021Matangazo
Mataifa ya Afrika Magharibi yanapambana kudhibiti uasi wa kijihadi katika eneo hilo, huku baadhi ya makundi yakionyesha utiifu kwa makundi ya kigaidi kama vile al-Qaida au lile linachojiita Dola la Kiislamu IS.
Shambulio la nchini Niger lililenga ngome inayotumiwa na nchi za ukanda wa Sahel kupambana na waasi.
Maafisa wamesema washambuliaji 79 na wanajeshi 29 wameuawa.
Washambuliaji waliokuwa katika pikipiki waliilenga kambi ya Fianto iliyoko katika mkoa wa Tillabéri.
Kambi hiyo inatumiwa na kikosi cha pamoja cha nchi za G5, ambacho kinajumuisha nchi tano za Sahel ambazo ni Mauritania, Niger, Chad, Mali na Burkina Faso.